Tuesday, April 12, 2011

HADITHI

Palikuwa na kijiji cha Mtunguchoya ,kata ya Legezamwendo,tarafa ya Madongokuinama,jamii ya zeruzeru, palikuwa na mzee mmoja aitwae mzee Toboamambo.Mzee Toboamambo alikuwa na watoto wawili Tototundu na Chongo.Mzee Toboamambo alichukiwa sana pale kijijini kwao kutokana na tabia yake ya kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji na vyombo vya dora kwa kila ovu aliloliona pale kijijini.

Viongozi wa halmashauri ya kijiji walimpenda sana mzee huyu kutokana na ushirikiano wake,Alikuwa mpenda maendeleo asiyeogopa kupigania maendeleo ya kijiji chake.Katika kijiji kile palikuwa na msitu mkubwa ulijulikana kwa jina la Takalang’onyo.Msitu huu ulikuwa mkubwa mno wenye vyannzo vya maji na kila rasilimali inayo patikana katika misitu.Msitu ulikuwa wakijani na ulitunzwa vizuri kutokana na mahitaji ya kimila ya jamii ya zeruzeru.Waliutumia msitu huu kwa kufanya shughuli za kimila kamavile matambiko,ibada za jadi na kwa mahitaji ya nyumbani kama vile kuni,kuchimba dawa za asili na matunda.Katika msitu ule kulikuwa na chanzo cha maji kikubwa ambacho kilitoa maji kwa kata nzima ya Legezamwendo.